GUMZO! Mkali wao kwenye
Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mtoto wa dada yake
Esma, Taraj wamezua gumzo la aina yake baada picha yao kutupiwa
mtandaoni na watu kudhani ni yule Tiffah wa Diamond ambaye hajawahi
kuonekana sura.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki
iliyopita baada ya Esma kuiweka picha inayomuonesha Diamond akiwa
amelala kitandani na Tahaj ndipo watu walipofikiri ni ya Tiffah na
kuanza kuijadili huku wengine wakitumiana kwenye simu zao wakijulishana
kuwa hatimaye ‘Tiffah’ ameonekana sura.
Kutona na gumzo kuzidi kukua kwa kasi,
sosi mmoja alimpigia simu mwandishi wetu na kumtumia picha hiyo
akimwambia ajionee Tiffah ameonekana sura.
“Mlikuwa mnahangaika kuipata sura ya Tiffah, huyo hapo sasa muangalie amwenyewe,” alisema sosi huyo.
Hata hivyo, mwanahabari wetu
alijiridhisha kuwa mtoto huyo si Tiffah bali Taraj wa dada yake Diamond
baada ya kuwasiliana na Esma mwenyewe.


Note: Only a member of this blog may post a comment.