SASA
imethibitika kuwa ndoa kati ya muigizaji nyota wa filamu Wastara Juma
na Mtangazaji Bond Suleiman itafanyika mara baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Bond
ambaye pia ni muigizaji, aliliambia gazeti hili kuwa wawili hao
wameshafikia muafaka wa kuoana lakini Wastara yupo bize na kampeni,
kwani baada ya kuanguka katika ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya CCM,
sasa anazunguka mikoani na Samia Suluhu ambaye ni mgombea mwenza wa John
Magufuli jambo ambalo limesababisha washindwe kufanya maandalizi.
“Unajua Wastara amejiingiza kwenye siasa
na mimi nataka akomae kwani itakuja kutusaidia baadaye ndiyo maana
tumekubaliana kuahirisha ndoa mpaka uchaguzi uishe ndipo tutapanga
tena,” alisema.
Note: Only a member of this blog may post a comment.