MASTAA wa Bongo Fleva, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na
mkali wa kibao cha Chekecha Cheketua, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’,
juzikati waligeuka kivutio ndani ya Uwanja wa Taifa, Dar mara baada ya
kuwasili wakiwa katika pozi la kimahaba, pasipo kujali macho kodo ya
mashabiki wa soka waliofurika uwanjani hapo.
Mastaa wa Bongo Fleva, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’
Tukio hilo lilijiri Septemba 26, mwaka huu ambapo wawili hao walikuwa
wameenda uwanjani hapo… …kushuhudia mechi ya watani wa jadi, Yanga na
Simba.Wawili hao wakiwa wameshikana kimapenzi bila wasiwasi walijumuika
pamoja na mashabiki wengine wa Yanga kuishangilia timu yao ambayo
iliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-0. Mmoja wa mashabiki wa Ali Kiba alisema hiyo ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuwaona wakiwa pamoja na kwa kweli walikuwa kivutio kikubwa kwake, kwani walikuwa kama mke na mume, tena sehemu kama ile.
Hata hivyo, inasemekana kuwa bifu hilo limemalizika kama meneja wa msanii huyo, Bude alivyothibitisha. “Ni kweli kulikuwa na tofauti kidogo lakini hivi sasa wapo pamoja.”
Jokate alipoulizwa kuhusu picha iliyowaonesha wakiwa wameshikana ndani ya uwanja huo, hakusema kitu badala yake, alirejesha jibu lenye alama ya mdomo unaobusu, kuonesha kuwa ni upendo tu!
Note: Only a member of this blog may post a comment.