Gabriel Ng’osha na Haruni Sanchawa
Eeh! Mungu tenda miujiza! Ni maneno ambayo
unaweza kuyasema ukimuona Mustapha Haruna (32), mkazi wa Ndala mkoani
Shinyanga anayesumbuliwa na tumbo kujaa maji baada ya moyo wake
kupanuka.
CHANZO CHA UGONJWA
Akizungumza na Uwazi,
kwa njia ya simu kutoka mkoani Shinyanga mama mzazi wa Mustapha,
Hidaya Mrisho alisema kuwa mwanaye alianza kuugua mwaka, 2005 baada ya
kusumbuliwa na miguu, kifua pamoja na homa kali.
Akizungumza na gazeti hili Hidaya alisema:
“Nilimpeleka Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, alipopimwa alibainika
kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu (TB) na kuanza kutibiwa, lakini
alihamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza ambapo
alipimwa na kugundulika kuwa moyo umepanuka na unamwaga maji tumboni na
kusababisha tumbo livimbe.
….Akiwa nyumbani kwake.
“Nimejitahidi kutumia kila namna ili kuokoa maisha yake lakini
nimeshindwa baada ya kuishiwa fedha, kwani ninatakiwa kumpeleka kliniki
Bugando ila sina uwezo zaidi ya kumpeleka hospitali ya mkoa wetu.
“Mara ya mwisho nilimpeleka kliniki mwaka 2010, tangu hapo sijawahi
kumpeleka kwa sababu ya kukosa fedha na kulazimika kumtibu hapa mkoani.
“Kutokana na tatizo alilonalo Mustapha, amewahi kutolewa maji machafu
lita 1 mwaka 2012 alipokuwa Hospitali ya Bugando na lita 5 mwaka 2014
akiwa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.
“Baadhi ya wataalam walinishauri kama nina pesa nimpeleke kijana
wangu India kwa matibabu zaidi, jambo ambalo siwezi bila msaada kwa
sababu kumpeleka Bugando tu, gharama zimenishinda.
MSIKIE MGONJWA
Akizungumza kwa tabu kijana Mustapha alisema:
“Kwa kweli naumwa; nakiona kifo hivihivi. Yeyote mwenye kuguswa na
tatizo langu naomba anisaidie kupata matibabu, fedha za dawa, chakula na
mengineyo ili niweze kurudi katika hali yangu, kwani kwa hali hii
nakiona kifo kikininyemelea.
“Nawaomba Watanzania waniepushe na roho wa mauti.”
Kwa yeyote aliyeguswa na tatizo la Mustapha
anaweza kuwasiliana naye kwa namba 0764420902, 0689837790 au namba ya
mama yake 0683952363 Hidaya Mrisho.
Note: Only a member of this blog may post a comment.