Baadhi ya wana CCM na wananchi wakiwa
wamefurika katika Viwanja wa Jitegemee Mjini Muheza ambapo mgombea
mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alifanya mkutano wa
kampeni jana.
Baadhi
ya wana CCM na wananchi wakiwa wamefurika katika Viwanja wa Jitegemee
Mjini Muheza ambapo mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu
Hassan alifanya mkutano wa kampeni jana.

Mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Usagara Tanga Mjini leo. Idadi kubwa ya wananchi walihudhuria mkutano huo hadi wengine kuzimia kutokana na msongamano.
Mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Usagara Tanga Mjini leo. Idadi kubwa ya wananchi walihudhuria mkutano huo hadi wengine kuzimia kutokana na msongamano.
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM
Kitaifa, Bi. Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi kwenye moja ya
mikutano ya kampeni za CCM timu ya mgombea mweza iliyofanyika mkoani
Tanga leo.
Baadhi ya vijana wakiwa wamepanda juu ya
gari ili kumsikiliza mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan
katika Jimbo la Mkinga.
Mgombea
mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimamishwa na wananchi
njiani alipokuwa akielekea katika Jimbo la Mkinga kufanya mkutano wa
kampeni.
Mgombea
mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimamishwa na wananchi
njiani alipokuwa akielekea katika Jimbo la Mkinga kufanya mkutano wa
kampeni.

Sehemu ya wanaCCM na wananchi ikiwa imemsimamisha barabarani mgombea
mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kumsikiliza alipokuwa njiani kuelekea
kwenye mikutano mikubwa ya kampeni.
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan amevunja ngome ya chama cha ACT
Wazalendo Mkoani Tanga pamoja na kuvuna wanachama 272 kutoka vyama
mbalimbali vya upinzani baada ya wanachama wa vyama hivyo kujiunga rasmi
na CCM.
Bi. Samia Suluhu ambaye ni mgombea
mwenza wa Dk. John Pombe Magufuli amefanikiwa kuvunja ngome za wapinzani
leo mjini Tanga katika mikutano yake ya kampeni baada ya wagombea
udiwani watano wa ACT Wazalendo kujiunga na CCM pamoja na wanachama
wengine 235 toka Tanga mjini kujiunga na CCM kwenye mkutano mkubwa wa
kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Usagara mkoani Tanga.
Akihutubia katika mkutano mkubwa wa
kampeni kunadi ilani ya CCM Tanga mjini uwanja wa Usagara, Bi. Samia
Suluhu aliwapokea wagombea udiwani watano kutoka ACT Wazalendo, wakiwemo
Wilson Elia (wa Kata ya Duga), Gasper Maboko (Kata ya Nguvumali),
Charles Luanda (Maweni) na Marry Scoty (Kata ya Tanga Sisi) pamoja na
Sada Mbwambo (viti maalum).
Mbali na madiwani hao kukihama chama cha
ACT, wanachama 235 kutoka ACT, CUF na Chadema walijiunga na CCM kwenye
mkutano huo wa Tanga mjini huku wengine 37 wakijiunga na CCM katika
mkutano mwingine ulofanyika Jimbo la Muheza hivyo kutimiza wanachama 272
wapya kujiunga katika mikutano ya siku hiyo.
Akizungumza na wanaCCM na wananchi
waliojitokeza mkutano wa Tanga Mjini, Bi. Suluhu aliwaomba kuichagua CCM
kurudi madarakani ili kuendeleza maendeleo iliyofikia katika maeneo
mbalimbali, ikiwemo huduma za kijamii na miundombinu hasa ya barabara.
Alisema wapinzani hawafai kupewa
madaraka kwa kuwa hawajajipanga kimfumo kwani hata viongozi wanaogombea
wamekimbia vyama vyao na wanachotaka ni maslahi yao zaidi. Alisema kwa
mkoa wa Tanga Serikali ya CCM imepanga kuyakagua mashamba makubwa
yaliotwaliwa na wawekezaji na kutelekezwa kisha kuyarejesha kwa wananchi
ili waweze kuyatumia kwa uzalishaji, ikiwa ni pamoja na kupanua bandari
ya mkoa huo kuchochea maendeleo.
Aidha aliongeza kuwa wakulima wa zao la
korosho hawana budi kuongeza uzalishaji na kutokata tamaa kwani tayari
Serikali inafanya mazungumzo na Serikali ya Norway kwa ajili ya ujenzi
wa kiwanda cha kubangua korosho mkoani hapo ili kuongeza thamani ya zao
hilo.
Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha
asilimia 40 ya vijana wanapata ajira kwenye viwanda vitakavyo jengwa
maeneo anuai ya nchi. Bi. Samia alifanya mikutano minne mikubwa katika
majimbo ya Mkinga, Pangani, Mheza na Tanga Mjini na mikutano midogo
midongo sita alioifanya njiani akisimamishwa na wananchi wakitaka
kumsikia alipokuwa akipita.
Hata hivyo katika mkutano wake wa Tanga
Mjini baadhi ya wananchi walizidiwa kutokana na msongamano na idadi
kubwa ya watu na kuzimia kabla ya kupewa huduma ya kwanza.
Gari ya Bi. Samia Suluhu ikitoka kwenye
kivuko cha Mv. Pangani II mara baada ya kuvushwa, mgombea huyo mwenza wa
urais CCM alikuwa akitoka kwenye mkutano wa hadhara JImbo la Pambani
leo.
Kutoka kushoto ni mgombea ubunge Jimbo la
Pangani, Jumaa Hamid Aweso, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Pangani, Hamis
Mnegero na Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan wakizungumza
jambo.
Aliyekuwa
mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na wanaCCM na
wananchi kwenye mikutano ya hadhara leo katika baadhi ya Majimbo ya Mkoa
wa Tanga.
Moja ya ahadi za CCM msimu wa Rais Jakaya Kikwete ikiendelea na ujenzi wa gati Wilayani Pangani ikiendelea na ujenzi
Bi. Samia Suluhu akishuka ndani ya kivuko mara baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Mwera Jimbo la Pangani.
Bi. Samia Suluhu akihutubia mkutano wa kampeni Muheza.
Baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM wakiwa katika msitari mara baada ya kurejesha fomu.
Sehemu
ya wanaCCM na wananchi ikiwa imemsimamisha barabarani mgombea mwenza wa
CCM, Bi. Samia Suluhu kumsikiliza alipokuwa njiani kuelekea kwenye
mikutano mikubwa ya kampeni.
Sehemu
ya wanaCCM na wananchi ikiwa imemsimamisha barabarani mgombea mwenza wa
CCM, Bi. Samia Suluhu kumsikiliza alipokuwa njiani kuelekea kwenye
mikutano mikubwa ya kampeni. 
Bi. Samia Suluhu akiwa na mgombea ubunge wa Jimbo la Tanga Mjini Omary Nundu(kulia).
Mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza Tanga Mjini leo.

Mgombea Ubunge wa CCM, Jimbo la Bumbuli, January Makamba akizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni.

Aliyekuwa
mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na wanaCCM na
wananchi kwenye mikutano ya hadhara leo katika baadhi ya Majimbo ya Mkoa
wa Tanga.

Mmoja wa wananchi wakipewa huduma ya kwanza mara baada ya kuzimia kutokana na msongamano katika mkutano wa kampeni kwa mbaya.
Note: Only a member of this blog may post a comment.