Magufuli akijinadi sambamba na mgombea ubunge jimbo la Ngara (CCM) Alex Gashaza.
Mgombea urais waJamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa awamu ya tao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.
Jonh Pombe Magufuli, jana amemaliza kufanya kampeni zake mkoani Kagera
kwa kufanya mkutano wa katika jimbo la Ngara lililopo wilayani Ngara.
Mkutano huo ulihudhuriwa na umati mkubwa wa watu ambao kwa mujibu wa
wenyeji, haijawahi kutokea watu kujaa kiasi hicho.
Sambamba na mkutano huo wa fungakazi,
Magufuli alifanya mikutano sehemu mbalimbali ikiwemo wilayani Misenyi
katika jimbo la Nkenge kwenye viwanja vya Mashujaa.
Mkutano mwingine mkubwa ulifanyika
viwanja vya Kayanga wilayani Karagwe, mkutano mwingine waliofurika umati
wa mkubwa wa watu ni ule wa Wilaya mpya ya Kyerwa, mwingine Kijiji cha
Kaishozi, Kijiji cha Kinyamisi kabla ya kumalizia na mkutano
uliofungakazi katika jimbo la Ngara ambapo Alex Gashaza anagombea
Ubunge.
Picha na Richard Bukos/GPL Kagera
Note: Only a member of this blog may post a comment.