Kwa umaarufu alionao mtoto wa Diamond na Zari, Latiffah Nasib Abdul
au kama baba yake anavyopenda kumuita Tiffah, ni wazi kwamba mashabiki
wengi wa staa huyo wangependa kumuona ama kumbeba mtoto huyo
aliyejipatia umaarufu toka siku yake ya kwanza duniani.
Hiyo inatokana pia na uamuzi wa wazazi wake kutomuonesha mapema sura yake hadi Jumapili iliyopita, ambayo iliongeza shauku hiyo.
Licha ya kuwa picha za kwanza kuonesha sura zake zilidhaminiwa na
makampuni, lakini Dimond amekanusha uvumi kuwa anatoza kiasi fulani cha
fedha kwa watu wa kawaida ambao wangepeda kumuona Tiffah uso kwa uso.
Diamond Ameiambia BBC kuwa habari hizo ni za uongo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.