Alikiba ameeleza kusikitishwa kwake kwa kile alichosemwa kupuuzwa kwa ushiriki wake kwenye kampeni ya Peace One Day iliyofanyika jana kwenye uwanja wa Amohoro jijini Kigali, Rwanda.
Alikiba aliungana na wasanii wengine wa Afrika wakiwemo Mafikizolo,
Ice Prince na wengine kuadhimisha siku ya kimataifa ya amani kwa
kutumbuiza wimbo wao maalum.
“Hii ni kwa vyombo vya habari ambavyo havijatoa ushirikiano katika kampani ya peace one day,” ameandika kwenye Instagram.
“Next time fanya kwaajili ya Tanzania sio kwasababu ya Alikiba au mtu
yoyote atakayewakilisha Tanzania kwasababu mimi ni binaadam
sijakamilika naweza kuwa nimekukosea bila kujua au kwa kujua pia.”
“Haijalishi kwasababu nchi yetu ina amani ndio muache kutoa
ushirikiano kumbukeni tupo kwenye kipindi kigumu cha uchaguzi naomba
Mungu atunusuru kwa hilo lakini pia inaleta picha mbaya kwa nchi za
jirani zenye machafuko kuona hatutoi ushirikiano,” ameeleza.
“Kwahiyo haipendezi kwa kweli. Kuna wapenzi wa kazi yangu
wamelalamika sana kila kona ya dunia kuhusu kampani ya peace one day
kwanini hamkuona hilo !! imeniuma.”
Note: Only a member of this blog may post a comment.