Rapper wa Afrika Kusini, Cassper Nyovest amesusia tuzo za 2015 MTV
Europe Music Awards (MTV EMA) kutokana na kuhisi kuwa hajatendewa haki.
Jumanne Sept 8, MTV walitangaza majina ya nominees 4 wa kipengele cha
‘Best African Act’ akiwemo Diamond Platnumz, na ikabaki nafasi ya
msanii mmoja ambayo waliweka majina ya wasanii watano wapigiwe kura
kupata mmoja wa kukamilisha nominees 5 wa kipengele hicho.
Wasanii waliowekwa kupigiwa kura na mashabiki kupitia Twitter kuwania
nafasi hiyo moja ni Wizkid (Nigeria), K.O (South Africa) Dj Arafat
(Ivory Coast), Stonebwoy (Ghana) pamoja na Cassper Nyovest (South
Africa).
Rapper huyo kupitia Instagram yake amesema, kutokana na kwamba
hakuchaguliwa kuwa nominee wa kipengele hicho bila kupigiwa kura kama
wasanii wenzake wakina Diamond, Davido, Yemi Alade na mpinzani wake
mkubwa AKA, basi anaona labda hakustahili nafasi hiyo hivyo haoni haja
ya kuomba kura ili achaguliwe kuwa nominee na ndio sababu ameamua
kujitoa.
“MTV just announced that I’m one of the people who have
to get people to vote for them to be nominated for Best African Act. As I
sit here and I think, It may be such an honor&an opportunity but if
I’m not nominated with all the other nominees that don’t HAVE 2 vote
then maybe I don’t deserve it. In that case, I have decided to stay out
of this one. Good luck to all of the nominees. I’d rather spend me time
trying to #FillUpTheDome!!! Shout out to all the fans that wanted to
vote&those that are already voting but let’s let this one go. Let’s
focus on filling up the dome!!!” – Cassper Nyovest
2015 MTV EMAs zitatolewa October 25 jijini Milan, Italy.

Note: Only a member of this blog may post a comment.