Rapper Young Dee amewataka wasanii wenzake kuacha kuoneana wivu baina yao kwa kuwa wote wanatafuta riziki kupitia muziki.
Young Dee aliiambia Planet Bongo ya EA Radio jana kuwa wasanii
wanatakiwa kuombeana dua kwa kuwa wote ni wamoja. “Mimi huwa naamini
kwamba as long as wote tunatafuta ugali kwa kutumia mic haina haja ya
kuoneana jealous,” alisema.
“Ni kuombea tu heri kila mtu afanikiwe katika sehemu yake anayofanya.
Mimi ni Young Dee na wengine wana majina yao na kila mtu ana brand
yake kama msanii,” alisisitiza.

Note: Only a member of this blog may post a comment.