Producer na msanii wa Navy Kenzo, Nahreel amekiri kuwa ngoma yao
‘Game’ ndio imefungua njia waliyohangaika kuitafuta kwa muda mrefu.
Ndani ya mwezi mmoja toka waiachie, ‘Game’ imeweza kukamata chati
mbalimbali za Radio na Tv sehemu nyingi Afrika. Imeshika namba moja
kwenye chati za vituo hivyo ikiwa ni pamoja na Top Ten East ya Soundcity
TV.
Akiongea na EATV Nahreel amesema kuwa tayari wamepata feedback
kutoka Nigeria, Ghana, Afrika Kusini, Zimbabwe, Kenya, na Uganda kuwa
‘Game’ inafanya vizuri sana kwenye nchi hizo.
Ameongeza kuwa matokeo hayo yametokana na bidii na juhudi waliyoiweka kwa muda mrefu.
Sept 9, Navy Kenzo walipost picha Instagram wakifanyiwa mahojiano na
Soundcity Tv ya Nigeria jijini Dar, ikiwa ni ishara ya kukubalika zaidi
Nigeria.
“Shukrani za dhati kwao @soundcityafrica kwa kufanya
maojiano na Navy Kenzo kuhusiana na muziki na nyimbo ya #Game ft
@vanessamdee kushika namba moja kwenye chat za #EastAfricaMusic..” – Navykenzoofficial

Note: Only a member of this blog may post a comment.