Malimi Busungu.
Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Malimi Busungu, amekumbwa na balaa baada ya hivi karibuni watu wasiojulikana kulitumia jina lake kwa lengo la kutaka kujinufaisha kiuchumi.
Matapeli hao wamekuwa wakilitumia jina hilo kupitia Mtandao wa Facebook ambako wamefungua akaunti mbili ambazo wamekuwa wazitumia kwa ‘kazi zao’ kinyume na sheria.
Akizungumza na Championi Jumatano, Busungu alisema kuwa hali hiyo kwa hakika imekuwa ikimkosesha amani kwani anaona kama imelenga kumchafua katika jamii.
“Nina zaidi ya miaka miwili sijaitumia akaunti yangu ya Facebook, hivyo ninashangaa watu hao wana nia gani na mimi.
“Akaunti moja inatumia jina la Malimi Busungu Ahmed na nyingine inatumia jina la Malimi Busungu tu, hivyo nawaomba watu wote wenye mapenzi mema na mimi wawe makini na watu hao, kwani ni matapeli,” alisema Busungu.
Note: Only a member of this blog may post a comment.