Beki wa Yanga Nadir Haroub “Canavaro” akiwania mpira na Kipa katika moja ya mechi za Ligi Kuu Bara.
Wilbert Molandi, Dar es Salaam
HUKU Ligi Kuu ya Tanzania Bara ikitarajiwa kuanza Jumamosi ijayo, timu tatu kubwa za ligi hiyo; Simba, Yanga na Azam, zimeonyesha kuwa jeuri yao hasa ipo kwenye ulinzi.
HUKU Ligi Kuu ya Tanzania Bara ikitarajiwa kuanza Jumamosi ijayo, timu tatu kubwa za ligi hiyo; Simba, Yanga na Azam, zimeonyesha kuwa jeuri yao hasa ipo kwenye ulinzi.
Hii inamaana kuwa, washambuliaji wanatarajiwa kupata ushindani
kutokana na ubora wa kila safu ya ulinzi, zaidi wanachotakiwa ni kuweka
mipango thabiti kuhakikisha wanafunga mabao, kwani safu za ulinzi za
timu hizo zimeonekana kuwa imara kila siku.
Championi limechambua rekodi za timu hizo za mechi za kirafiki na
michuano ya Kombe la Kagame iliyozishirikisha Yanga na Azam FC, huku
Simba wakionekana kuwa bora kutokana na mechi zao za kujipima nguvu.
Hassan Kessy.
Simba
Yenyewe imecheza michezo kumi ya kirafiki katika kujiandaa na ligi kuu
chini ya Kocha Mkuu Muingereza, Dylan Kerr, akisaidiana na Selemani
Matola.
Katika michezo hiyo ya kirafiki, Simba ambayo imekuwa ikiwatumia mabeki
wake Juuko Murushid, Hassan Isihaka, Mohammed Husein ‘Tshabalala’ na
Hassan Kessy, imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara tano tu.
Simba iliruhusu mabao kwenye michezo dhidi ya JKU walipolala 2-0, Simba 2-1 Polisi Zanzibar na Simba 3-2 KMKM.
Hiyo imeonyesha jinsi gani timu hiyo imefanya kazi nzuri kwenye safu hiyo ambayo ni mhimili mzuri wa timu.
Mbali na kuokoa, pia beki wao Murushid ameonekana kuwa bora kwa kufunga
kama alivyofanya kwenye mchezo dhidi ya Sports Club Villa ya Uganda.
Kwa wastani, hii ni safu nzuri ya ulinzi ambayo inaweza kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri msimu huu.
Pascal Wawa.
Yanga
Chini ya Kocha Mkuu Mholanzi, Hans Pluijm, wamecheza michezo 11, kati ya
hiyo wameruhusu nyavu zao kutikiswa mara tatu tu dhidi ya Gor Mahia
waliyokutana kwenye Kagame ambayo walifungwa mabao 2-1 na dhidi ya
Kimondo FC waliyoshinda 4-1.
Safu ya ulinzi ya Yanga imeonekana kuwa bora kutokana na mabeki wa kati
wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani, huku pembeni
wakicheza Haji Mwinyi na Mbuyu Twite unaweza kuitaja kuwa ndiyo safu ya
ulinzi yenye uzoefu wa juu kuliko nyingine zote kwenye ligi hii.
Katika kikosi hicho, Cannavaro ameonekana mhimili mkubwa kutokana na
silaha kubwa anayoitumia ya kuokoa mipira ya krosi na kona kwa kutumia
kichwa chake, pia anasifika kwa kufunga mabao kwa njia ya kichwa.
Safu hii ni tishio sana na washambuliaji ambao wanaweza kuipita hakika watatakiwa kufanya kazi kubwa.
Azam FC
Hauwezi kuitaja safu ya ulinzi ya Azam bila ya kumtaja Muivory Coast,
Serge Pascal Wawa ambaye kwenye michuano ya Kombe la Kagame ametwaa
uchezaji bora kwenye michezo mitatu.
Wawa akiwa anaichezea timu hiyo pamoja na Aggrey Morris, wamecheza mechi
12 mara baada ya msimu uliopita kumalizika, kati ya hiyo wameruhusu
mabao mawili tu yote kwenye mechi za kirafiki huku wakimaliza michuano
ya Kagame bila kuruhusu bao.
Azam waliruhusu mabao hayo mawili kwenye mechi na JKT Ruvu ambayo
walifungwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya
Dar es Salaam.
Katika mchezo mwingine ambao Azam waliruhusu bao ni ule waliovaana na Ndanda ambapo walitoka sare ya bao 1-1.
Timu hiyo imeruhusu mabao hayo mawili ikiwa tayari imecheza michezo tisa mfululizo bila ya kufungwa bao lolote.
Safu hiyo ya ulinzi ya Azam, inamtegemea zaidi Wawa ambaye kama
akikosekana ni pengo kubwa kutokana na aina yake ya ukabaji akiwa ndani
ya uwanja ambayo inawatisha washambuliaji wa timu pinzani na
uhamasishaji wake kwa wachezaji wenzake wakati wanatafuta ushindi.
Lakini pia amekuwa akisaidiana na Morris, Shomari Kapombe pamoja na
Erasto Nyoni, hii ni safu nyingine ya ulinzi yenye uzoefu wa hali ya
juu.
Note: Only a member of this blog may post a comment.