Thursday, August 27, 2015

Anonymous

SEHEMU YA 4: Sababu za Wanaume Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa!

libidoladies13132
Baada ya wiki iliyopita kuelezea mambo kadhaa yanayosababisha wanaume kukosa hamu ya tendo la ndoa, leo nitaelezea tatizo la kuwahi kufika kileleni Katika vitu ambavyo wanaume wengi hawapendi vijulikane na wenzi wao ni tatizo la kuwahi kufika kileleni.

Kila mwanaume hupenda aonekane ni rijali au mwanaume kamili mwenye uwezo wa kushiriki tendo la ndoa bila shida yoyote. Na imezoeleka katika jamii zetu ikiwa mwanaume atakuwa ana tatizo la kuwahi kufika kileleni anaweza akatangazwa mtaa mzima kila mtu ajue, hali hii husababisha aibu kubwa na fedheha.

Katika mazingira kama hayo mwanaume mwenye tatizo hilo hata kama hajatangazwa na mwenzi wake amemtunzia siri hiyo, anajihisi kuwa hafai. Hali hii humfanya kila anapopata hamu ya kushiriki tendo la ndoa aogope kushiriki kuhofia ataabika. Hii ina mchango mkubwa sana katika kumfanya mwanaume apoteze hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

Tumekuwa tukiangalia tatizo la wanaume wengi kushindwa kushiriki tendo la ndoa. Tumeangalia jinsi tatizo hilo linavyoisumbua jamii yetu na pia tumejua kuwa mwanaume kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa si jambo la kawaida ni tatizo linaloweza kutibika. Zifuatazo ni njia za kuondoa tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Wengi wanatarajia kuambiwa wameze dawa fulani ili kuondokana na tatizo hilo. Kama una tatizo hilo ni vema ukawaona matabibu kwa ushauri na uchunguzi ili kujua chanzo chake na upate matibabu. Ni vema kwa wanaume wenye tatizo hilo washirikiane na wake zao ili kuliondoa.

Katika nchi zilizoendelea, wataalam wamekuwa wakigundua dawa na vifaa tiba vipya vya kuondoa tatizo hilo na vingi bado ni vya bei kubwa na/au vinapatikana kwa shida. Vipo ambavyo vimeonesha mafanikio makubwa, mifano ya vitu hivyo ni Suction Vibrators, Desire Creams na Erection Drugs.

Habari njema ni kwamba tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa mimea na matunda tiba ya kawaida ambayo ipo katika mazingira yanayotuzunguka.

Utafiti umeonesha kuwa tunachokula ndicho kinachotujenga na kutufanya tuwe watu wa aina gani. Vyakula tunavyokula vina mchango mkubwa katika kujenga au kubomoa afya zetu hivyo ni muhimu kuwa makini katika kuamua tule nini na tunywe nini. Kuna uhusiano mkubwa kati ya chakula tunachokula na afya ya viungo vya uzazi.

Baadhi ya chakula na virutubisho vimehusishwa na hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
Usikose kufuatilia Alhamisi ijayo kwenye gazeti hilihili.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.