Huenda sio Flaviana Matata pekee aliyeolewa weekend hii. Inaonekana
kuwa muimbaji wa ‘Kaniganda’ Meninah naye amefunga pingu za maisha japo
kimya kimya!
Habari zilisambaa kuwa Jumapili hii, Meninah alifunga ndoa na ameendelea kupongezwa na watu wengi kwenye mtandao wa Instagram.
Meneja wa muimbaji huyo ambaye pia ni kaka yake, Atick amethibitisha kuwa ni kweli dada yake ameolewa.
“Yeah ni kweli ameolewa Meninah, mengine siwezi kuongea zaidi ya jibu hilo basi,” amesema Atick.
Kama ni kweli, tunampongeza Meninah kwa hatua hiyo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.