WEMA Sepetu ‘Madam’ ameangusha dua ya
nguvu nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar ikiwa ni maalum kwa ajili ya
kumshukuru Mungu kwa ushindi wa rais mteule wa awamu ya tano wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.
Dua
hiyo ilifanyika juzi na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali walioshiriki
kwenye kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo baada ya kumalizika
kwa dua hiyo pamoja na kula chakula, Madam alisimama na kuzungumza:
“Wasanii wenzangu wakumbuke kusoma dua kila Mungu anapowabariki kufanikisha mambo yao. Namshukuru sana, tumezunguka nchi nzima, Mungu katuepusha na ajali na pia mgombea wetu Magufuli ameshinda.” Miongoni mwa wasanii waliohudhuria shughuli hiyo ni pamoja na Snura Mushi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’.
Note: Only a member of this blog may post a comment.