Msanii wa filamu Rose Ndauka amesema alishangazwa kuona wasanii wengi
wakijitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wakati wameshindwa
kuisimania tasnia ya filamu.
Ndauka ameiambia Bongo5 kuwa alitegemea kuona wasanii wakiwekeza
nguvu zao ili kuboresha umoja wao. “Mimi kiukweli nilishangaa wasanii
wote kugombea, sio tu mmoja wote. Lakini pale pale niliwapongeza kwa
sababu walithubutu, kwa sababu ndani yao wameona wana vitu vya
kuwafanyia watu wao,” alisema.
“Kitu ambacho kilinishtua nadhani bado tasnia yetu ya filamu
inayumba. Nilikuwa nategemea wasanii wengi wawekeze nguvu zao kwenye
tasnia yetu ya filamu na kuibadilisha kuitoa sehemu moja na kuipeleka
sehemu nyingine, hicho ndicho kitu ambacho nilikuwa nategemea mimi.
Kwahiyo sikushtuka kwa nia mbaya, nilishituka kwa sababu nilikuwa na
mawazo yangu binafsi kwamba kuna siku wasanii watajitokeza kwa wingi kwa
pamoja na tukashikamana kuibadilisha hii tasnia,” aliongeza.
Note: Only a member of this blog may post a comment.