Muimbaji wa Yamoto Band, Aslay amesema kumweka wazi mpenzi wake kumempunguzia usumbufu kwa kiasi kikubwa.
Aslay ameiambia Bongo5 kuwa alitumia njia hiyo ili kuwapunguza wasichana waliokuwa wakimnyemelea.
“Unajua sisi ni public, wengi wanakuangalia kwa mtazamo tofauti,
lakini kwa upande wangu uamuzi wa kumweka mpenzi wangu wazi kila mtu
amjue kimenisaidia sana,” amesema.
“Sasa hivi sisumbuliwi kabisa, mambo ya ndoa bado ila tuombe Mungu tu wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi.”
Note: Only a member of this blog may post a comment.