Thursday, August 27, 2015

Anonymous

PICHAZ: MAGUFULI AFANYA MKUTANO WA KIHISTORIA MKOANI MBEYA....Shuhudia Hapa!


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia c\Chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tunduma waliofurika kwa wingi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma,mkoa wa Mbeya mapema leo mchana,kwenye mkutano wa kampeni wa kuwaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano,ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyia Oktoba 25 mwaka huu.



Wananchi wakimsikiliza Magufuli

Maelfu ya Wananchi wa Tunduma waliojitokeza kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika uwanja wa shule ya msingin Tunduma mkoani Mbeya

Wananchi wakiwa wamefurika katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchama kumsikiliza mgombea urais wa CCM akimwaga sera zake kuwaomba Watanzania wamchague na kumpa ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa kwa shangwe na wananchi alipokuwa akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana kwa ajili ya mkutano wa kampeni

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.