Thursday, August 27, 2015

Anonymous

Miaka 14 tangu kifo cha AALIYAH: Nuru the Light amuelezea jinsi alivyokuwa msanii wa pekee

August 25, miaka 14 iliyopita, mwanamuziki mrembo wa Marekani, Aaliyah alipoteza maisha kwenye ajali mbaya ya ndege alipokuwa akitokea kushoot video ya wimbo wake ‘Rock the Boat’ kwenye visiwa vya Bahamas.
page
Aaliyah (kushoto) na Nuru the Light (Kulia)
Mastaa mbalimbali duniani jana walimkumbuka staa huyo ikiwa ni pamoja na Janet Jackson aliyeandika kwenye karatasi: “What I shared with u [is] ever sacred, everlasting [and] it’s pure and it will endure. I love u Aaliyah. #RIP.”

Naye mwanamuziki wa Tanzania mwenye makazi yake nchini Sweden, Nuru Magram maarufu kama Nuru the Light amemzungumzia Aaliyah kama muimbaji aliyekuwa na maisha ya aina yake.

Nuru alitilia mkazo kile kinachoaminika kwa watu wengi nchini Marekani kuwa kama Aaliyah angekuwa hai Beyonce asingekuwa msanii mkubwa kama alivyo leo.
“She was very humble halafu alikuwa msanii ambaye anajua anachokifanya japo alianza akiwa mdogo, but I think alikuwa na timu nzuri, nadhani hicho ndicho kilichomsaidia sana,” Nuru alikiambia kipindi cha The Jump Off cha Times FM Jumanne hii.

“Kwasababu alikuwa na timu nzuri ambayo iliweza kumlinda, iliweza kumpanga, iliweza kumtungia kazi nzuri ili asikike dunia nzima, na alikuwa mtu ambaye ‘she is lovable, yaani alikuwa sio mtu wa makelele sana, she was very humble and very quiet,” aliongeza.

“Ni huzuni kwamba alifariki wakati bado there was a lot to do, lakini sometimes hayo ndio maisha hatujui Mungu ana sababu zake.”
Nuru alikuwa akitambulisha wimbo wake mpya uitwao L. Unaweza kumsikiliza kwa kubonyeza HAPA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.