Miss Tanzania 2011, Salha Israel
Miss Tanzania 2011, Salha Israel kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa
tangu aingie kwenye ndoa na Abdulatif Fundikira, ametulizwa kwa kiasi
kikubwa.Akizungumza na Amani, Salha alisema kwa sasa ameachana na mitoko isiyokuwa na mpangilio pamoja na kucheza filamu kutokana na mumewe kutopendezewa.
“Unajua nimeolewa na familia ya Kiislamu ambayo mambo ya filamu na vitu vingine hawapendezwi navyo. Kwa sasa hata nguo fupi sijui zinavaliwaje kila kitu kimebadilika katika maisha yangu,” alisema Salha.
Salha aliolewa na Abdulatif mwishoni mwa mwaka jana baada ya mumewe huyo kuachana na mwanamitindo, Jack Patrick ambaye yupo kifungoni Macau, China.

Note: Only a member of this blog may post a comment.