Msanii wa filamu Bongo, Lungi Maulanga
amefunguka kuwa, kuna mmoja wa wagombea udiwani katika Jimbo la
Kinondoni jijini Dar, (jina linahifadhi kwa sasa) amekuwa akimsumbua
kila siku akitaka ampe penzi.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni,
Lungi alisema mwanasiasa huyo amekuwa na tabia ya kuwarubuni mastaa wa
kike na hivi karibuni alishangaa akimpigia simu na kumtaka wakutane.
“Mimi nilishangaa aliponipigia simu
usiku na kuniambia ana shida ya kuonana na mimi. Sikujua alipata namba
yangu kwa nani ila kwa kuwa namjua ni mpenda totoz, nilimwambia
haitawezekana.
“Kuanzia siku hiyo imekuwa ni usumbufu
tu, nimefikia hatua ya kufunguka ili kama anasoma hili gazeti ajue
akiendelea nitamuanika, sipendi kusumbuliwa kwa kuwa nina mtu wangu
anayeniweka mjini,” alisema Lungi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.