Shauku ya wanawake wengi kuitwa mama ni
kubwa sana, namaanisha kwamba kuwa na mtoto ni moja ya heshima ambayo
wanawake wengi wanaililia, walio kwenye ndoa na hata wale walio nje ya
ndoa.
Lakini wakati uhalisi ukiwa hivyo,
vitendo vya kutoa mimba vimekuwa vikiripotiwa kila siku. Baadhi ya
wanawake wamekuwa wakijisahau na kujikuta wamenasa bila kutarajia kisha
kukimbilia kutoa. Huu ni uuaji!
Na niseme tu kwamba, kama uliwahi kutoa
mimba, tubu kwa Mungu wako, kama una mimba na unataka kuitoa, achana na
mawazo hayo na kama hujawahi kushika mimba bila kutarajia, kuwa makini
kuanzia sasa.
Kwa nini leo nAyaandika haya?
Anahisi hatazaa tena
Kwa maelezo yake Wema anasema kuwa,
tangu afanye hivyo imekuwa ni ngumu kwake kushika mimba wakati sasa
anatamani sana awe na mtoto wake.
“Mimi napenda sana watoto, kila mtu
anajua hilo na napenda siku moja niwe na wa kwangu. Tumehangaika sana
mimi na Diamond (Nasibu Abdul) kutafuta mtoto lakini ilishindikana,
ikafika wakati nikiziona siku zangu naumia. Nimehangaika hosptalini,
nimetumia kila aina ya dawa lakini wapi.
Anahisi kutoa mimba kumechangia
“Wakati mwingine nahisi labda ‘abortion’
imefanywa vibaya kiasi cha kwenda kuharibu vitu huko ndani. Nilitoa
mimba kwa kuwa sikuwa tayari kupata mtoto, nilikuwa mdogo na pia ndiyo
kwanza nilikuwa nimeingia kwenye penzi.”
Ni laana ya Kanumba?
Wema anaeleza kuwa, Kanumba hakupenda
kile kitendo cha kutoa mimba yake na hata kabla ya kifo chake kuna
wakati alikuwa akimtania kwa kumwambia ana deni lake.
“Aliniambia kuwa ananidai na kwamba
atafanya vyovyote nimrudishie watoto wake. Sasa huenda labda mzimu wake
ndiyo unaosababisha haya yote,” anaeleza Wema kwa masikitiko.
Umejifunza kitu?
Ushuhuda huu wa Wema ni lazima uwe fundisho kwa kila mwenye ndoto ya kuitwa mama.
Leo unaweza kupata mimba, ukasema bado
hauko tayari kuzaa, ukaitoa! Kumbe hiyo hiyo ndiyo ilikuwa chansi pekee
na matokeo yake ikawa ndiyo basi tena.
Wema anafikiria hivyo lakini pia huenda
ikawa tofauti na kile anachodhani kwani yawezekana ni mtihani tu ambao
Mungu anampa ili ampime imani yake.
Lakini pia wapo wanawake ambao mpaka leo
wanateseka kwa kutopata mimba kutokana na laana za wapenzi wao. Endapo
uko kwenye uhusiano au ndoa, ukapata mimba na mwenza wako akafurahi
kisha kwa sababu unazozijua wewe ukaitoa, chozi lake haliwezi kukuacha
salama.
Mwanaume ataumia kwa kuifuta ndoto yake
ya kuitwa baba na manung’uniko yake yanaweza kuwa laana kwako. Ndiyo
maana Wema anasema, chozi la Kunumba huenda ndilo linalomtesa mpaka leo
hii.
Neno kwa Wema
Hatakiwi kukosa furaha kwa kutoshika
mimba. Ni kweli baada ya kutoa ile mimba ya Kanumba alihangaika sana
kutafuta mtoto akiwa na Diamond lakini huenda Mungu hakupenda azae naye.
Cha kufanya ni kumtafuta mtu ‘siriasi’
wanayeweza kuanzisha familia kisha ajiachie aone kama hatanasa. Wakati
mwingine hofu zinatufanya tukose amani kwa mambo ambayo huenda muda wake
bado.

Note: Only a member of this blog may post a comment.