Mfanyabiashara anayedaiwa kusababisha kifo cha mjumbe huyo.
MAJONZI! Mjumbe wa nyumba kumi, Lucas Bahati Kinuma, (60) ambaye pia
ni fundi mitambo mstaafu wa Kituo cha Runinga cha ITV na mkazi wa Goba
jijini Dar ameuawa na majambazi kwa kupigwa risasi nne za tumbo
alipokuwa akitaka kunusuru uhai wa mfanyabiashara, Japhet Mshani.Tukio hilo la kutia simanzi, lilitokea Agost 20, mwaka huu saa moja usiku nyumbani kwa Lucas.
Akizungumza na Amani kwa masikitiko nyumbani kwake, Goba jijini Dar, Japhet alisema kuwa alikuwa akielekea nyumbani kwake lakini kabla hajafika alikutana na kundi la majambazi sita wakiwa wamevaa vitambaa usoni huku mikononi wakiwa na silaha.
“Nilichukua uamuzi wa kushuka kwenye gari na kuanza kutembea ili wasijue kama naishi maeneo yale, kitendo cha kushuka, majambazi wanne kati ya sita walibaki wakiulizana na kusema kwamba mtu mwenyewe ndiye huyu, nilivyosikia vile nikaanza kukimbia mpaka kwa mjumbe huku nikipiga mayowe (mjumbe majambaziii) nikiamini wakisikia neno mjumbe wataogopa,” anasema Japhet.
Mke wa mfanyabiashara huyo.
Japhet anaendelea kusimulia kwa masikitiko kuwa alipofika kwa mjumbe
wale majambazi nao tayari walikuwa wameshafika, wakaanza kuvutana
wenyewe kwa wenyewe huku yeye akiendelea kuomba msaada kwa mjumbe.“Mjumbe alifungua mlango na kuanza kubishana nao na huo ndiyo ukawa mwanya wa mimi kuingia hadi chumbani.
“Baada ya muda, mjumbe naye aliingia akafunga mlango na kwenda moja kwa moja hadi dirishani kwake kwa lengo la kuwafukuza kwa maana bado walikuwa nje. Kitendo cha kutaka kuwafukuza kupitia eneo la dirishani, palepale milio ya risasi ikarindima na baada ya muda kimya kikatanda,” anaendelea kusimulia Japhet kwa majonzi.
Japhet anasema, majambazi hao waliondoka na kuelekea nyumbani kwake na kumkuta mama yake mzazi, Matrida Mbughi akianua nguo ndipo wakamshika na kumwambia awaoneshe mahali alipo mwenye nyumba huku wakimpiga mwilini kwa kutumia panga, kishoka na kirungu wakitaka wapewe fedha.
“Eva aliingia chumbani kwenda kutoa pesa yote ya mauzo ya siku hiyo na kuwakabidhi, wakasema mbona inaonekana ni hela ndogo sana niwaongezee nyingine nikachukua funguo na kwenda dukani kuangalia kama kulikuwa na pesa wakakuta kuna vocha ambazo zilikuwa zimetoka kununuliwa jioni ile zenye thamani ya laki saba nazo wakabeba.
Mwili wa marehemu Lucas ulizikwa nje ya nyumba yake siku ya Jumapili.
Imeandaliwa na Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani.

Note: Only a member of this blog may post a comment.