Idadi ya wasanii wa Tanzania wanaotuwakilisha kimataifa inazidi
kuongezeka, pongezi kwa WEUSI kwa kuamua kujitoa kwa dhati na matunda ya
jitihada zao yanaonekana.
Msanii anayeipeperusha vizuri bendera ya Tanzania nje ya mipaka,
Diamond Platnumz amefurahishwa na juhudi za Weusi katika kujitangaza
kimataifa, ukizingatia ndio wasanii wa Hip Hop ambao nyimbo zao zimeanza
kupewa nafasi kwenye runinga na radio za kimataifa zikiwemo Trace Urban
na MTV Base.
Hayo hayakuja hivi hivi, mpaka pale Joh makini na wenzake kwa juhudi
zao binafsi walipoamua kuwekeza na kwenda kushoot video ya ‘Nusu Nusu’
Afrika Kusini, na matokeo tayari tumeanza kuyashuhudia.
Hit maker wa ‘Nana’ amempongeza Joh Makini na Weusi ambao
wamekamilisha kushoot video 2 ikiwemo ile ya collabo yao na rapper AKA
wa Afrika Kusini.
Diamond ndiye aliyemleta AKA kwenye Zari All White Party jijini Dar
mwezi May mwaka huu, na baada ya AKA kutua ndio Joh alipata nafasi ya
kurekodi naye wimbo. Hivyo kwa sehemu kubwa pia Diamond amehusika katika
kufanikisha collabo hiyo ambayo soon tutaanza kuiona katika runinga.
Kupitia Instagram hiki ndicho Diamond amekiandika kuhusu Weusi na harakati zao;
“Halaf kweli kesho na Kesho kutwa mtu anakuja anasema Ooh flani
freemason ooh mara flani Sjui Anabebwa, ooh sjui Anaroga wakati mtu
anaHaso na kujituma 24/7 kila mtu anaona…. mi nakuheshim sana
@joh_makini na Team yako nzima ya WEUSI kwa juhudi na Harakati zenu za
kilasiku mnazozizidisha…Mwenyez Mungu Aendelee kuwasmamia na
Kuwabariki.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.