Christian Bella amesema anajipanga kumpeleka mtoto wake wa kiume kwenye shule za mpira nchini Sweden.
Bella ameiambia Bongo5 kuwa anajisikia fahari kumchagulia mwanae
kwenda kwenye shule za mpira kwa kudai mchezo huo unalipa sana kwa nchi
za Ulaya.
“Unajua mzazi ndio mtu pekee anayeweza kumpeleka mtoto wake sehemu
salama,” amesema muimbaji huyo. “Ndio maana mimi nikaona nikimpeleka
mwanangu kwenye shule za kucheza mpira nitakuwa nimemsaidia sana. Mpira
unalipa sana Ulaya.”
“Unajua baba yake ni mwanamuziki na naamini pale alipo ndani yake ana
chembechembe za muziki, lakini nikaona tu nimtafutie kitu kingine
ambacho pia kinaweza kuwa bora,” aliongeza.

Note: Only a member of this blog may post a comment.