Thursday, August 20, 2015

Anonymous

BREAKING NEWS: MANCHESTER UNITED YAPIGWA DAFRAO TENA LEO...CHELSEA WAFANYA YAO RASMI KWA KIFAA HIKI TOKA FC BARCELONA!

Habari nyingi kwa sasa katika michezo ni kuhusiana na usajili wa wachezaji mbalimbali ndicho kitu kinacho weka headlines kubwa katika vyombo vya habari, ilikuwa ni kuhusiana na Pedro Rodriguez kuhamia katika klabu ya Manchester United kabla ya dili hilo kubadilika.
Pedro-as-a-Chelsea-player
Usiku wa August 19 zilianza kuandikwa tetesi kuwa Pedro atajiunga na klabu ya Chelsea na sio Man United kama ilivyoandikwa awali katika vyombo vya habari na kuwa walikubaliana bei, habari zimethibitika kwa Pedro kujiunga na Chelsea kwani alipewa ruhusu na FC Barcelona August 18 ili kwenda London kufanya vipimo vya afya.
p2
Masaa 11 pekee yalitosha kuipiku Man United katika mbio za kusaka saini ya nyota huyo hivyo Pedro amethibitisha kuwa London kwa ajili ya vipimo vya afaya na anafuraha kujiunga na ChelseaFC Barcelona na Chelsea wamekubaliana uhamisho wa euro milioni 30 ila kuna uwezekano wa kuongezwa euro milion 3 kulingana na kiwango atakacho onyesha Pedro. Pande zote mbili zimethibitisha uhamisho huo wa Pedro.
p
“Nafuraha kuwa hapa na nina furaha kuanza kuitumikia Chelsea na nipo hapa kuendeleza kutwaa mataji shukrani kwa klabu na mashabiki kwa kunipa nafasi ya kuvaa jezi ya Chelsea “>>>Pedro
p3

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.