Thursday, August 27, 2015

Anonymous

AY awachukua Hermy B na Marco Chali kwenye mradi mpya

AY amewachukua Hermy B na Marco Chali kutengeneza ngoma yake mpya.
11252465_1647628742120195_616091842_n AY akiwa studio na producer wa B’Hits, Hermy B na producer wa MJ Records, Marco Chali
AY ameshare picha hiyo juu akiwa studio na watayarishaji hao wakubwa nchini wanaowakilisha studio maarufu zaidi, Hermy B wa B’Hits na Marco Chali wa MJ Records.
Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza AY anakutana tena studio na Hermy B baada ya kuwahi kupishana katika masuala ya kibiashara mwaka 2012.Baada ya hapo AY amekuwa akifanya kazi zaidi na Marco. 

“Unategemea kitu kitatokaje?? Best Producers @marcochalitz & @hermyb kwenye chumba kimoja na Mzee wa Commercial.. BIT TINGZ R GWAN!! #ZEE #ElCapo #FAYAAAA #KofiazaMarcoChali,” ameandika AY.
Mashabiki wameonesha kufurahishwa mno na picha hiyo na matarajio yao ni makubwa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.