Hamilton, New Zealand
PAKA mmoja huko Hamilton nchini Uholanzi
amegundulika kuwa na mchezo mchafu wa kuiba nguo za majirani na soksi
hasa wakiwa wamelala usiku wa manane.
Taarifa zilizotolewa na mmiliki wa paka
huyo, Sarah Nathan zimeeleza kuwa katika kipindi cha miezi miwili, paka
huyo mwenye umri wa miaka sita ambaye anayejulikana kwa jina la Brigit
aliiba nguo za ndani za ndani (boxer) 11 na zaidi ya soksi 50. Cha
kushangaza ni kuwa, paka huyo huiba nguo za ndani za wanaume pekee.
Sarah Nathan aliandika ujumbe unaoelezea
tabia ya paka huyo isiyo ya kawaida katika mtandao wake wa facebook na
kueleza kushangazwa kwake na tabia hiyo huku akianika wazi namna ambavyo
paka huyo amekuwa akimpa wakati mgumu hasa anaporudi nyumbani na
vifurushi vya nguo alivyoiba huko mtaani.
”Tabia hiyo sasa inazidi kuwa mbaya. Lazima kuna mtu ambaye anakosa
vitu vyake”, alisema katika ujumbe wake kwenye ukursa wa facebook
lililosambazwa mara 500.
Bi Nathan ameeleza kwamba tatizo la paka huyo kuwa mwizi lilianza
alipogundua vipande kadhaa vya nguo za ndani katika nguo zake
anapoziosha.
Tangazo lililowekwa na Sarah Nathan kuhusu wizi wa paka huyo.
”Nguo hizo za ndani hazikuwa zetu, na siku moja Brigit aliingia
katika chumba cha wageni (nyumbani kwa Nathan) akiwa amebeba soksi”,
akisema kuwa waathiriwa wa Brigit walikuwa majirani katika nyumba za
ghorofa.
Note: Only a member of this blog may post a comment.