Joseph Haule aka Profesa Jay atawania ubunge katika jimbo la Mikumi, Morogoro kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
Tulikutana naye kwenye tuzo za KTMA 2015 Jumamosi iliyopita na akatueleza kile anachoweza kufanya kuwasaidia wasanii wenzake.
“Nitakachoanza nacho, sio kwenda kutetea hoja za wasanii,” alisema.
“Nitakachoanza nacho na kinachotufelisha siku zote ni wasanii kutokuwa na umoja. Kwahiyo nitapambana kuhakikisha wasanii wanakuwa na umoja wao ili zile changamoto zetu tulizonazo tuanze kuzipanga kwa kipaumbele. Kwasababu sasa hivi utaratibu uliopo ni kwamba kila msanii analia kwa kilio chake, mwingine anasema soko limekuwa bovu, mwingine anasema mapromota wanawasumbua, mwingine anasema serikali haiangalii masuala ya piracy.
Lakini kitu ambacho kinaendelea ni kwamba tunatakiwa tuwe na kauli moja ili wasanii wote tukisema tunataka tuangalie haki zetu za msingi tuseme haki. Tukisema nyimbo zetu tunataka zipigwe redioni tukilipwa wote tukiwa kitu kimoja. Kwahiyo unity ni kitu cha msingi na nitaanza na unity kabla ya kuendelea na utaratibu mwingine.’

Tazama video hiyo hapa chini tafadhali....

Note: Only a member of this blog may post a comment.