Saimeni Mgalula, Mbeya
Ukatili kila kona!
Mwanamke aliyetajwa kwa jina la mama Joy amechezea kipigo ‘hevi’ kutoka
kwa wananchi wenye hasira kali akidaiwa kumchoma moto mikononi mtoto
anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka saba ambaye jina halikupatikana kwa
madai ya kumuibia shilingi elfu ishirini.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya mashuhuda walisema kuwa mtoto huyo alikuwa akiishi katika mazingira magumu almaarufu kwa jina la chokoraa hivyo hana makazi maalum.
Walifunguka kuwa mara baada ya kuwa na maisha hayo, ilibidi mama Joy amuombe aishi naye ambapo mtoto huyo alikubali na kuacha kulala nje ya nyumba na udokozi kwa kuwa alikuwa anapata chakula.
Walidai kwamba, baada ya kusikia hivyo, baadhi ya wananchi wenye hasira kali walianza kumbonda mama Joy huku wakimkokota kuelekea Kituo cha Polisi Tunduma ili sheria ichukue mkondo wake.
Hadi gazeti hili ‘linaanua matanga’ eneo la tukio mama huyo alikuwa ameshikiliwa polisi huku mtoto huyo akipelekwa hospitalini kwa matibabu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.