KIWANGO! Tofauti
na watu wengine ambao maumbile yao hubadilika mara baada ya kujifungua,
kwa staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel hali imekuwa tofauti, uzuri
na umbo lake limebaki vilevile.
“Nachukia ubonge nyanya, namshukuru Mungu pia kwani wengi wakijifungua huwa wananenepa hovyo lakini kwangu mambo yamekuwa tofauti. Niko vilevile, nafikiri pia ni kutokana na kufuata ushauri mzuri wa kula chakula niliopewa,” alisema Aunt.
Mbali na kutobadilika, Aunt alisema kwa sasa muda mwingi anautumia kuwa nyumbani na ubavu wake, Moze Iyobo wakimlea mtoto wao tofauti na zamani alipokuwa na misele ya usiku katika viwanja tofauti vya starehe.

Note: Only a member of this blog may post a comment.