Stori: Gladness Mallya na Musa Mateja
BAADA ya
hivi karibuni kunaswa akiingia katika jengo lao, staa mwenye mvuto
kunako gemu la filamu Bongo, Jacqueline Wolper amezidi kugandwa na
skendo ya Jamii ya Siri (Secret Society) ya Freemason akidaiwa kuishi
kwa masharti ya taasisi hiyo huku nyumba yake ikiwa imejaa vitu
vinavyodaiwa kuwa vya ‘Ki-freemason’.
“Akiamka (Wolper) saa kumi hiyo alikuwa akinikataza nisiamke, sikuwahi kujua huwa anafanya kitu gani akiamka na kwa nini alikuwa akinikataza, ukweli maisha yake anaishi kwa masharti ya ajabuajabu nahisi ni Freemason,” alisema dada huyo.
Dada huyo alitaja kuwa nyumbani kwa mwigizaji huyo, Mbezi Beach jijini Dar, kumesheheni mapambo kibao ya Kifreemason ambayo huyatunza na kuyalinda kama binadamu hali ambayo ilikuwa ikimpa wakati mgumu kwani hakuwahi kuona mambo kama hayo maishani mwake.
Dada huyo alitoa picha za vifaa vya ndani kama saa, picha za ukutani vyenye alama zinazodaiwa kuwa za Freemason pamoja na picha ya mwili wa Wolper ambayo imechorwa alama zinazodhaniwa kuwa ni za jamii hiyo ya siri.
Na huu ukiwemo.
Baada ya kupata habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Wolper ambaye alijibu kwa kifupi;“Ni kweli huwa naamka saa kumi lakini ni kwa ajili tu ya kufanya mazoezi, kuhusu hayo mengine napenda tu picha na vitu vyenye nembonembo sasa mimi sijui kama ndizo za Freemason.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.