Ni kama kumekucha! Tayari mbinu za
kuchafuana na kupakana matope miongoni mwa wanasiasa waliojitokeza
kugombea urais kupitia chama kimoja cha siasa zimeanza kujitokeza baada
ya hivi karibuni kuibuliwa kwa picha ya mgombea mmoja wa chama hicho
aliyetangaza nia akiwa na hawara ndani ya chumba cha hoteli.
Kuibuliwa
kwa picha hiyo kumekuja siku chache kufuatia mgombea huyo kutangaza nia
huku akianika kipaumbele chake endapo atapata ridhaa ya wapiga kura
kuingia ikulu.
MUDA WA PICHA
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichotinga katika
Ofisi za Global Piblishers, Bamaga-Mwenge, inadaiwa kuwa, mheshimiwa
huyo (jina tunalo) na mwanamke huyo ambaye si mke wake, walipiga picha
hiyo muda mrefu lakini kutokana na duru za kisiasa za uchaguzi mkuu
mwaka huu, picha hiyo inaonekana kuwa ‘keki’ kwa wapinzani wake.
“Unajua hii picha ni ya muda mrefu. Mheshimiwa alipiga akiwa na
uhusiano na huyu mrembo. Sasa mheshimiwa alipotangaza nia tu, wabaya
wake wakaona hapa ndiyo penyewe, wakaiibua ili itumike kwenye kampeni
yake ya urais kama chama chake kitampitisha yeye kugombea,” kilisema
chanzo hicho.
ENEO LA PICHA
Ilizidi kudaiwa kuwa, picha hiyo ilipigwa ndani ya hoteli moja maarufu
iliyopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam na mpigaji alikuwa mwanamke
huyo ambaye hakujulikana jina akitumia simu yake ya mkononi kwa kuishika
kwa mkono wake wa kulia (selfie).
SI MKE WAKE
Chanzo kilisema kwa sababu mheshimiwa huyo wa kutoka
Kanda ya Ziwa ana mke na watoto na anaheshimika katika jamii, kupiga
picha ya namna hiyo kunamuondolea sifa ya kuwa rais wa Tanzania.
“Ingekuwa
picha yenyewe ni mheshimiwa na mke wake, sidhani kama wabaya
wangeitumia lakini sasa si unajua maadili ya Kiafrika. Nadhani hata
wenzetu nje, huwezi kuwa na mke halafu ukawa na hawara wakakupa cheo
kikubwa kama cha urais wa nchi,” kilisema chanzo hicho.
HALI ILIVYO KWA SASA
Tayari baadhi ya wagombea wa urais kupitia
vyama mbalimbali wameanza kuwalilia baadhi ya wenzao kwamba, wameanza
kucheza rafu katika safari ya kinyang’anyiro cha kuusaka urais kwa
kuwatafutia skendo chafu, za zamani na mpya ili wachafuke katika jamii
na kuonekana hawafai kukabidhiwa ikulu, Oktoba mwaka huu.
ORODHA YA WAGOMBEA
Mpaka sasa, mbali na Chama Cha Cuf ambapo wameshamtaja Profesa Ibrahim
Lipumba kugombea urais mwaka huu, wanachama wenye nguvu walioonesha nia
ya kugombea nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni Edward
Lowassa, Benard Membe, Frederick Sumaye, Samuel Sitta, Makongoro
Nyerere, Mwigulu Mchemba, Lazaro Nyalandu, January Makamba ambapo baadhi
yao picha zao zimetumika ukurasa wa mbele wa gazeti hili.
Saturday, June 13, 2015
PICHA YA UTUPU YA MGOMBEA URAIS TANZANIA AKIFANYA YAKE NA MCHEPUKO YAIBULIWA
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Filed Under:
UDAKU
on Saturday, June 13, 2015

Note: Only a member of this blog may post a comment.