Khadija Mngwai, Dar es Salaam
MUDA wowote kuanzia sasa, Simba itamsajili beki wa pembeni anayemudu kucheza kushoto na kulia, Amili Miboma pia timu hiyo imewatema baadhi ya wachezaji wake akiwemo Issa Rashidi ‘Baba Ubaya’.
Dili la Simba na beki huyo raia wa Burundi nchi anayotokea straika wa Yanga, Amissi Tambwe, limefikia patamu na mambo yakienda vizuri Miboma atasaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo kwa miaka miwili ijayo.
Mmoja wa mabosi wa Simba anayetumiwa kufanya usajili katika hatua za mwisho, aliliambia Championi Jumamosi kuwa, beki huyo anasajiliwa ili kumaliza tatizo la ulinzi wa pembeni. “Huyu beki yupo Burundi na anachezea Vital’O, tayari ameshatumiwa mkataba na muda wowote atakuja nchini ambapo atasaini,” alisema bosi huyo.
Hata hivyo, Simba tayari inao mabeki Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ upande wa kushoto na kulia yupo Hassan Kessy.
Wakati huohuo, Simba imepanga kuachana na wachezaji Baba Ubaya, Nassor Masoud ‘Chollo’, Miraj Adam, Abdalah Seseme na Ibrahimu Twaha na itatangaza kuwaacha muda wowote. Habari kutoka ndani ya Simba zinasema wachezaji hao wataachwa kwa wale ambao mikataba yao imeisha na wenye mikataba watapelekwa mahali kwingine kwa mkopo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.