Tuesday, April 21, 2015

Anonymous

SIRI IMEFICHUKA: HII NDIO SABABU YA MZEE MOYO KUTIMULIWA CCM

Anaandika KAROLI VINSENT
SIRI ya kufukuzwa mwanasiasa mkongwe nchini na muasissi wa siasa za maridhiano Zanzibar, Hassan Nassor Moyo (pichani)ndani ya chama cha mapinduzi CCM zimeanza kufichuka na sababu hiyo inadaiwa kutokana na uswahiba wake wa karibu na Edward Lowassa.Mtandao huu umedokezwa)

Taarifa toka visiwani Zanzibar zinasema Mwanasiasa huyo mkongwe kabisa ndani ya CCM ambaye alishiriki kukianzisha 5 Februari 1977,inadaiwa ukaribu wake wa Mbunge wa Monduli CCM,Edward lowassa unadaiwa kumponza na sio madai ya usaliti wa kwenye chama hicho kama yanavyosema .

Mzee Moyo alitimuliwa uanachama ndani ya Chama hicho juzi kwa madai ya kung’an’ngania mfumo wa muungano wa Serikali tatu ambao chama chake wamekuwa wakiupinga sana.

Kwa mujibu wa Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi, Aziza Mapuri alisema sababu ya kumfukuza mwanasiasa mkongwe inatokana na kuzingatia Ibara ya 93(14) ya Katiba ya CCM.

Taarifa ambazo Mtandao huu ambazo umezipata leo asubuhi na mapema zinasema sababu ya kufukuzwa Mzee moyo ambazo zinadaiwa na CCM ni za uongo kwani sababu halisi ni inatokana na kuwa na ukaribu na Mwanasiasa ambaye amekuwa akisumbua chama chake kutokana na nguvu aliyekuwa nayo katika kutaka kuchukua nafasi ya Urais hapo baadae mwaka huu ambaye ni Edward Lowassa. 

Lowassa ambaye ni Waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi kwenye Kampuni Tata ya Richmound ni miongoni mwa makada ndani ya CCM ambao wanataka Urais kwa udi na Uvumba.
Akifichua sababu ya kumfukuzwa mzee Moyo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM (NEC) ambaye pia ni Mjumbe wa kamati CC kutoka visiwani Zanzibar,akiongea na Mtandao huu kwa sharti la kutotaja jina lake amesema Chama chake kinaficha ukweli tu kwani inajulikana wazi kwamba ukaribu wake na Lowassa ndio umemponza.


“Sikufichi bwana anachokizungumza bwana Mapuri ni kuwadanganya watu tu ,kwani huyu mzee ni siku nyingi sana amekuwa akishikilia msimamo wa Serikali tatu,iweje wamfukuze leo na sio nyuma,na sisi tunajua kwamba huyo mzee aliaapa kumpigania Lowassa kuchukua nchi hii,ndio maana wamemuengua mapema na hapa wanafanya ubabe tu”kimesema Chanzo hicho.

Mjumbe huyo amendelea kuongea kwa uchungu anasema kwa sasa chama hicho chini ya Mwenyekiti Jakaya Kikwete ni kama kinaongozwa kwa mfumo ambao anadai ni wa kibabe.

“Chama hichi kilipofikia sasa ni wazi kinakuwa ni cha kibabe sana haiwezekani mtu ukimpenda mtu na ukimtaka agombee Urais unapingwa na kufukuzwa uanachama,wakati wakiwa kwenye majukwaa wanasema tuwashawishi tuwafuate watu wenye sifa na tuwaombe wagombee uongozi lakini tukifanya hivyo tunabwanwa”ameendelea kusema.

Mzee Moyo ambaye asili ya baba yake ni Songea, mkoani Ruvuma, mwenyewe akiwa amezaliwa mjini Zanzibar, miaka 81 iliyopita, amekuwa na wake wawili, mmoja mjini Zanzibar na wa pili jijini Tanga na ukaribu wake na Lowassa unadaiwa kuchagizwa sana na kile kinachonekana mwanasiasa huyo kwamba lowassa atakuwa mtu mwajibikaji na kukubali muundo wa Serikali tatu ambao Kada huyo mkongwe wa CCM anasema unateweza kuwatoa wa Zanzibar kwenye mfumo kandamizi wa Serikali mbili.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.