Tuesday, April 21, 2015

Anonymous

BENKI YA STANBIC YASHINDWA KUTOA MAJINA YA VIGOGO WALIOCHOTA PESA ZA ESCROW!

Taarifa za ndani ya Stanbic zinadai kuwa benki hiyo imeshindwa kutaja majina ya waliochota mabilioni ya Escrow kwa Malumbesa na Rambo. Taarifa hizo zinadai kuwa, pamoja na kuwepo kwa nia hiyo, benki hiyo ilikumbana na vikwazo vya ndani na nje ya benki hiyo hadi kukubali kukaa kimya. Ilipangwa kuwa,majina ya waliochota mabilioni ya Escrow kupitia miamala ya Stanbic yangewekwa hadharani hadi kufikia Aprili 1,2015.

Hata hivyo, Stanbic inadaiwa kuwatimua kazi wafanyakazi mbalimbali waliohusishwa na miamala hiyo iliyokuwa na harufu na tuhuma za ufisadi. Wafanyakazi hao ni wa ngazi na kada mbalimbali ndani ya Stanbic. Huu ndiyo mwisho wa filamu ya kujulikana kwa waliochota mabilioni ya Escrow kwa lumbesa na rambo? Tujipe moyo!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.