Mwamvita Makamba ni mtoto wa Mzee Yusuf Makamba na ni dada wa Naibu Waziri January Makamba ambaye amekua akitajwa kwa uzito kwenye headlines za uchaguzi mkuu wa Tanzania 2015.
Stori kwenye headlines hivi karibuni
Mwamvita aliandikwa na baadhi ya magazeti kwamba baada ya January
kutajwa kwenye headlines za uchaguzi mkuu, Mwamvita avamiwa na watu
wenye silaha Johannesburg Afrika Kusini.
Baada ya hizo headlines kuendelea Mwamvita anaefanya kazi na kuishi Afrika Kusini alikubali kuongea kwenye Exclusive interview na millardayo.com na kusema >>> ‘Hii haihusiani na January kugombea
Urais na wala haihusiani na uvamizi unaofanywa kwa wageni Afrika
Kusini, ilikua ni ajali tu imenikuta nikisafiri kutoka Johannesburg kwenda Sun city jioni’
>>>
‘Nilipita eneo ambalo mchana Polisi walituambia kulikua na maandamano
kwahiyo jioni ile walikua wamebakia wahuniwahuni wachache lakini sisi
hatukuona sababu ilikua usiku, wakati tunapita mbele yetu ndio tukaona
vijana wamechoma matairi’
>>>
‘Nikajaribu kugeuza gari upesi ili nirudi tulikotoka lakini wale vijana
wakaanza kutukimbiza, wakarusha mawe kwenye gari, mmoja akafyatua
risasi lakini tuliweza kukimbia…. risasi na mawe yote yakagonga kioo
changu cha nyuma cha gari ambacho ndio peke yake kimevunjika, tulikua
wawili tu mimi naendesha na nilikua nimempa lift Mfanyakazi mwenzangu’
>>>
‘Lilikua ni tukio la dakika 5 tu lakini ilikua hatari sana sababu wale
vijana wengine walikua wameshafika kwenye kioo changu pembeni yani
walikua wameshalizunguka gari, tunamshukuru Mungu tuko salama na hakuna
aliyejeruhiwa’ – Mwamvita Makamba.
Unaweza kumsikiliza Mwamvita kwa kubonyeza play hapa chini..
-via millardayo

Note: Only a member of this blog may post a comment.