Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima,amesema haogopi mtu yeyote wala kufa bali ataendelea kuinyoosha nchi anapoona haiendi sawa.
Kwa mujibu Askofu Gwajima, baadhi ya watu wamekuwa wakimhusisha kuwa na urafiki na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowasa jambo ambalo alikiri ni la ukweli kwa sababu walifahamiana tangu mwaka 1996.
“Niliwahi kumuita Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara nne hapa ili aje
azindue moja ya kazi zangu,hakuja badala yake nilimuita Lowassa na
aliitikia wito wangu na kuja kuifanya kazi hiyo hivyo siwezi kumuacha.
“Wapo
viongozi wengi ambao wanakuja kusali katika kanisa langu, kwa mfano
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye, kwa nini wasimseme yeye
badala yake wanamsema Lowasa tu?.
“Nashangaa mnatoka mlipotoka mnaongea kwa kubana pua, ukimuogopa mtu
nchi itakuwa haiendi vizuri na mimi sitaogopa kukemea mambo ambayo
hayafai katika jamii, mfano suala la Escrow.
Katika ibada hiyo aliliombea Taifa
amani, uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu na kikao
kijacho cha Bunge la Bajeti linalotarajia kuanzia baadaye mwezi ujao.
Wiki iliyopita, Askofu Gwajima
alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mashitaka mawili
ambayo ni kumtolea lugha ya matusi ambayo imemfedhehesha Askofu Mkuu wa
Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, na kuweka vibaya silaha anayomiliki.

Note: Only a member of this blog may post a comment.