Saturday, February 7, 2015

Anonymous

SHUGHULI PEVU: DONDOO MUHIMU ZA MECHI ZOTE ZA LEO LIGI YA ENGLAND #EPL

Shughuli pevu wikiendi hii Ligi kuu England
Ligi Kuu England itaendelea tena wikiendi hii ambapo michezo saba ya mzungo wa raundi ya 24 itapigwa katika viwanja tofauti.
katika uwanja wa White Hart Lane, Tottenham wataikaribisha Arsenal kwenye Dabi ya London ya Kaskazini, Arsenal wako nafasi ya tano wakiwa na pointi 42 huku Tottenham wakiwa nafasi ya sita kwa pointi 40.

Alexis Sanchez atakosa mchezo huu kutokana na kuwa majeruhi huku mshambuliaji Dany Welback atakua anarejea baada ya kuwa nje ya uwanja toka mwezi Desemba.
Vinara wa ligi hiyo Chelsea watashuka dimbani kuwakabili Aston Villa huku timu hiyo ikiendelea kukosa huduma za mshambuliaji wake Diego Costa.

Man City walioko nafasi ya pili kwa alama 48 alama 5 nyuma ya vinara Chelsea wao watakua na kibarua cha kuwania alama tatu muhimu kwa kuwakabili Hull city.

Majongoo wa jiji Liverpool watachuana na wapinzani wao wakubwa Everton katika kuwania pointi tatu muhimu.

Michezo mingine itakua ni kati ya timu inayoburuza mkia Leicester City dhidi ya Crystal Palace, huku QPR wakishuka dimbani kuwakabili Southampton, Swansea na Sunderland.

Mchezo wa mwisho wa ligi hiyo kwa siku ya Jumamosi utakua ni kati ya Everton na Liverpool.

England - Premier League
15:45
Tottenham Hotspur  ? - ? Arsenal

18:00
Aston Villa  ? - ?  Chelsea

18:00
Leicester City ? - ? Crystal Palace

18:00
Manchester City ? - ? Hull City

18:00
Queens Park Rangers ? - ? Southampton

18:00
Swansea City ? - ? Sunderland

20:30
Everton ? - ? Liverpool
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU TENA!
-BBC SWAHILI

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.