Dan Sserunkuma.
Na Richard Bukos, TangaGUMZO kubwa jijini hapa ni mtanange wa kukata na shoka kati ya wakongwe wa soka nchini, Simba watakaovaana na Coastal Union leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkwakwani katika mechi ya Ligi Kuu Bara.
Utamu wa mechi hiyo unatokana na mazingira yake na upinzani uliopo kati ya timu hizo, hasa ikikumbukwa kuwa katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar, Simba ilitangulia kupata mabao mawili kupitia kwa Shaaban Kisiga na Amissi Tambwe lakini Coastal wakayarudisha yote kupitia kwa Yayo Lutimba na Ramadhani Salim.
Lakini bado mashabiki, wachezaji na viongozi wote wa Simba wanakumbuka kuwa kwenye mechi ya kwanza msimu huu dhidi ya Coastal, straika wao Mkenya Paul Kiongera aliumizwa goti na hajarejea Msimbazi hadi leo, hatua ambayo inalifanya pambano hilo lisubiriwe kwa hamu kuona nini kitatokea.
Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic na msaidizi wake, Selemani Matola, jana na juzi jioni walikuwa na kazi ya ziada ya kuwapika wachezaji wao kujiandaa na mechi hiyo lakini msisitizo zaidi ulielekezwa kwa watu wawili.
Kopunovic amekuwa akiweka msisitizo katika ufungaji na zaidi anaelekeza nguvu zake kwa Dan Sserunkuma na Emmanuel Okwi katika mbinu za kuhakikisha mabao yanapatikana.
Pamoja na hayo, kocha huyo aliwaingizia mbinu nyingine mastraika wake tegemeo, Sserunkuma na Okwi, kwani alikuwa akiwaonyesha jinsi ya kumzunguka adui na kuachia mashuti makali ya kiufundi, ambapo alianza kwa kufanya yeye mwenyewe matukio hayo kwa vitendo kisha kuwapa nafasi hiyo wachezaji.
Jana katika Uwanja wa Popatlal mbele ya umati mkubwa, kocha huyo mwenye makeke mengi, alikuwa akitoa maelekezo ya wachezaji wake kupiga mashuti ya karibu na mbali.Wachezaji walioonekana kuwa vinara kwenye zoezi hilo la mashuti ni Dan Sserunkuma, Simon Sserunkuma na Okwi.
Msimamo wa ligi kuu unaonyesha kuwa Simba ina pointi 16 na inashika nafasi ya nane huku Coastal ikiwa nafasi ya saba ikiwa na pointi 17.Lakini ikumbukwe kuwa, kwenye Uwanja wa Mkwakwani msimu uliopita timu hizo zilitoka suluhu huku Simba ikipigwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Shakira ameonyesha picha za mtoto wake aliyejifungua!
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU
TENA!
===>>SOMA ZAIDI HAPA!


Note: Only a member of this blog may post a comment.