Thursday, April 7, 2016

Anonymous

Muda Mwingine Wanaume Kuchapiwa Wake zetu Tunatakaga Wenyewe!

Hili suala nimelifikiria kwa kipindi kirefu sana., naona mifano mingi kupitia kwa marafiki zangu na hata ndugu zangu na watu wangu wa karibu. Unakuta mwanaume upo kwenye mahusiano ya kawaida na msichana bado hamjafunga ndoa alafu migogoro na kuachana mara kwa mara, tena unakuta wewe ndo unaachwa na huyo mwanamke alafu unambembeleza mnarudiana. Mwanamke haonyeshi upendo wowote kwako lakini wewe unaendelea kumpenda na kumjali sana. Hayo yote haujifunzi unaamua kumng'ang'ania na mwisho wa siku mnafunga ndoa.

Hivi mwanamke kama huyo akiwa anakusaliti katika ndoa utamlaumu nani.?
Kuna rafiki yangu wa karibu aliwahi kuoa mwanamke wa aina hiyo, ndoa yao ilidumu kwa miaka 5 tu na mimi nilikuwa best man wake, maana mwisho wa siku ikaja kugundulika hata watoto wawili ambao walikuwa wameshazaa hawakuwa wa kwake.

Wanaume tujifunze jamani tunapochagua mwanamke wa kuishi naye kwa maisha yote, tusiziendekeze akili za nyege wakati wa kuchagua wenzi wa maisha.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.