Thursday, April 7, 2016

Anonymous

MENGINE YA KUMKUMBUKA STEVEN KANUMBA LEO APRIL 7

Na Zuhura Simba
Ni Miaka minne sasa tangu nyota wa Tasnia ya Filamu Nchini Seven Kanumba alipofariki dunia Tarehe 07/04/2012 akiwa nyumbani kwake Sinza Vatcan jijini Dar es Salaam.
Ilikuwa siku ya Majonzi na huzuni sio tuu kwa watanzania bali hata wasio watanzania kutokana na wasifu wake kwenye kazi zake za uigizaji.

Steven Kanumba alikuwa Zaidi ya Mwigizaji kwa maana ya kuwa na uwezo mkubwa na ubunifu kwenye kazi zake,jambo ambalo lilimfanya akubalike na watu wa aina zote bila kuzingatia Umri,Dini na Kabila.

Watu kutoka maeneo mbalimbali walijiotokeza na kuweka idadi kubwa ya watu zaidi ya 30,000.
Marehemu kanumba aliwahi kufanya kazi za maigizo zifuatavyo katika luninga kama Jahazi,Dira, Zizimo, Tufani, Sayari, Taswira, Gharika na Baragumu katika kituo cha Televisheni cha ITV.

Katika enzi za Uhai wake aliwahi kutoa filamu kama Haviliki, Neno, Ulingo, Riziki, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, My Sister, Penina, Cross My Sin, A Point of No Return ,The Lost Twins,The Stolen Will,Village Pastor, Magic House, Oprah, Red Valentine, Family Tear , The Movie’s Director, Fake Smile, Unfortunate Love , Hero Of The Church,Saturday Morning, Shauku, Crazy Love, 2006 Johari , 2006 Dar 2 Lagos, 2010 More Than Pain, 2010 Young Billionaire, 2010 “Ripple of tears”, 2010 Uncle JJ, 2010 This Is It, 2010 Off Side , 2011 Deception, 2011 Devil Kingdom , 2011 The Shock, 2011 Moses, 2012 Big Daddy, 2012 Because of you na Ndoa Yangu, Filamu ya mwisho ni Love and Power.

Na pia alikuwa Muongozaji wa Filamu kama, Mr Bahili, Kaka Benny, Lango La Jiji, Papara , 2010 Young Billionaire.
Mwaka 2006 Aliwahi kupata Tuzo ya “Muigizaji Bora wa Mwaka“, Mwaka 2007 kutokana na juhudi zake kwenye Tasnia ya Filamu alifanikiwa kupata tuzo ya “Muigizaji Bora wa Tanzania” na ilipofika Mwaka 2007/2008 alipata tuzo ya “Msanii Bora wa Mwaka“.  

“Mungu akupumzishe kwa amani na Mwanga wa Milele umuangazie,Amina“.
Siku ya Leo Wasanii na watu mbalimbali kupitia mitandao ya Kijamii na wengine wameandaa Misa katika makanisa ili kuendesha ibada ya kumuombea Steven Charles Kanumba ili apumzike kwa amani kwenye nyumba yake ya milele.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.