Wednesday, March 9, 2016

Anonymous

SIMBA SC Yakimbilia Jeshini!

Kikosi cha Simba.
Omary Mdose na Said Ally
KIKOSI cha Simba jana asubuhi kilikuwa kikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko jijini Dar, lakini ghafla kilikatisha mazoezi yao kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wakati huo.
Simba ilikuwa ikifanya mazoezi hayo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa kesho Alhamisi dhidi ya Ndanda FC na walipokatisha wakapanda basi lao na kuelekea Ndege Beach kwa ajili ya kambi kabla ya mchezo huo. 

Championi Jumatano lililokuwepo mazoezini hapo, liliwashuhudia wachezaji hao wakifanya mazoezi, lakini wengine hawakufanya kutokana na matatizo mbalimbali.
Wachezaji waliokosekana jana mazoezini ni Mussa Mgosi, Ibrahim Ajib, Peter Manyika, Hassan Kessy, Mohammed Fakhi na Hija Ugando.

Meneja wa timu hiyo, Abbas Ally, aliliambia Championi Jumatano kuwa kambi hiyo iliyoanza jana Jumanne ni maalum kwa mchezo dhidi ya Ndanda na inategemea na matokeo watakayoyapata kwani wanaweza kuendelea nayo au la.

“Baada ya mazoezi wachezaji wote wanaelekea kambini kuiwinda Ndanda, tutakaa huko mpaka mchezo wetu utakapoisha, baada ya hapo tutaangalia jinsi matokeo yatakavyokuwa, kama tukishinda tunaweza kuwapa mapumziko ya siku moja wachezaji wetu, lakini kama tukipoteza basi haina haja ya kupumzika, tutaendelea na mapambano ya kuwania ubingwa,” alisema Ally.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.