Na Richard Bukos, Risasi Mchanganyiko
STAA wa filamu za Kibongo aliyeshinda
tuzo katika African Magic Viewers Choice Awards ‘AVCA’ katika kipengele
cha Filamu Bora ya Mwaka kupitia Filamu ya Kitendawili, Single
Mtambalike ‘Richie’ mwishoni mwa wiki akiwasotesha vilivyo mastaa
waliokwenda kumpokea ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar alipokuwa akirejea kutoka Lagos, Nigeria.
Tukio hilo la kumpokea lilifanyika usiku
wa Jumapili iliyopita ambapo mastaa kibao walikwenda ‘airport’ kumpokea
Richie na kujikuta wakimsubiri kwa muda mrefu.
“Yaani Richie ametusotesha kweli maana alisema watawasili kuanzia saa nne lakini angalia mpaka saa saba hii ndiyo wanafika, ukweli tumechoka lakini tunampongeza kwa sababu amerudi na tuzo kwani hii ni sifa kubwa kwetu waigizaji wa Kibongo,” alisema kiongozi huyo.
Richie akiwa na tuzo yake mkononi alichomoza kwenye mlango wa abiria wanaowasili mishale ya saa saba za usiku ambapo mkewe, Asha Salehe, alishindwa kujizua na kumrukia kama anapiga mbizi na kumchum, kisha kumvalisha shada na baadaye tukio la kulishana keki iliyoandaliwa na TAFF lilifuata kwa watu mbalimbali.
Akizungumza kwa furaha uwanjani hapo, Richie aliwashukuru wote waliofika kumpokea muda huo na kuwaambia kuwa kitendo hicho kimemuongezea faraja na kumpa ari ya kujituma zaidi.
Aidha alisema Watanzania sasa wameshajitambua na kuondokana na dhana potofu ya kizamani kuwa mabingwa wa kuigiza filamu katika Bara la Afrika ni Wanigeria na mataifa mengine ya magharibi.
Note: Only a member of this blog may post a comment.