Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm (kulia) akiongea na kocha msadizi, Juma Mwambusi.
Nicodemus Jonas, Kigali
KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amesema wanachotaka katika mechi yao ya kesho Jumamosi dhidi ya APR ni kushinda.
KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amesema wanachotaka katika mechi yao ya kesho Jumamosi dhidi ya APR ni kushinda.
Yanga itakuwa mgeni wa APR katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Amahoro jijini hapa, kesho Jumamosi.
Akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya Yanga kutua
jijini hapa, Pluijm amesema wamelenga kushinda ili kujiweka katika
mazingira mazuri kabla ya mechi ya pili.
“Niseme tumekuja hapa kwa kuwa tunataka kushinda, tunajua ugumu wa mchezo utakavyokuwa na tunawaheshimu APR kama timu nzuri.
“Niseme tumekuja hapa kwa kuwa tunataka kushinda, tunajua ugumu wa mchezo utakavyokuwa na tunawaheshimu APR kama timu nzuri.
“Tunajua pia wamefika katika hatua hii baada ya kuitoa timu kama
ilivyokuwa kwetu, lakini sisi tunataka ushindi na tutapambana,” alisema
Pluijm.
Wachezaji wa Yanga walionekana kuwa ni wenye furaha na wanaojiamini kwa kiasi kikubwa. Yanga imefikia katika hoteli ya kisasa ya The Mirror ambayo ipo karibu kabisa na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali.

Note: Only a member of this blog may post a comment.