Thursday, December 22, 2016

Unknown

Jela Miaka 30 Kwa Kubaka Mtoto wa Miaka Tisa Jijini Dar

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, Shabani Hussein (29) baada ya kupatikana na hatia ya kubaka mtoto wa miaka tisa.

Hussein amehukumiwa kifungo hicho baada ya mahakama kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi watano. Hukumu hiyo imetolewa Jumatano hii na Hakimu Mkazi, Catherine Kihoja baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Catherine alisema “Kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapa umeweza kunithibitishia shitaka hivyo mshtakiwa ninamtia hatiani kama alivyoshitakiwa,”alisema Hakimu Catherine.

Aidha Hakimu aliongeza kuwa upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi watano ambao wameweza kuthibitisha shitaka hilo pasipo kuwa na shaka yoyote.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.