Ligi kuu ya Tanzania bara inaendelea na sasa iko katika mzunguko wa lala salama na mechi ya pili tayari zimechezwa kama ilivyokawaida saa moja lililopita tuliangalia Yanga namna ilivyo sawa kila idara leo sasa zamu ya Mnyama Simba na kocha wao Omog wapi inaelekea na namna gani ya soka linachezwa Simba.
Bila ya ubishi Simba inacheza kandanda safi sana msimu huu, kila mmoja anatamani aone kile Simba wanakifanya kiwanjani kwa maana ya pasi safi pamoja na kuonana, huenda wakawa hawana mshambuliaji kamili haswa baada ya kuondoka kwa Ibrahim Ajib akisaka tobo mbele wakati Mavugo akionekana anazingua haswa kuwa mchoyo wakati akitaka kumalizia kufunga lakini pia mzito. Kwa wapenzi wa timu hiyo wanaonekana kabisa hawana mpango nae japo kocha ndio muamuzi wa hatma ya mchezaji kiwanjani.
SIMBA WANACHEZAJE?
Kwa sasa kocha Omog anatumia sana viungo na jopo zima kuanzia kati hadi mbele anatumia viungo pamoja na winga ili kupata matokeo na bahati nzuri anapata kweli matokeo, kumtumia Mohamed Ibrahimu kunampa faida ambapo ndiye aliyevaa viatu vya Ibrahimu Ajib na analeta madhara kwa wapinzani.
Ila kunapokuwa na mazuri lazima mabaya yawepo wengi wanajiuliza kwanini Said Ndemla anakosa nafasi wakati kama anatumia viungo huyu mtu anaweza kukupa vitu 2 kwa wakati mmoja, hilo swala si letu sisi waongeaji mwalimu ndio anaujua uzuri au ubaya wa Ndemla, lakini angalia alivyoingia katika mechi ambayo Ruvu Shooting wamekufa bao 1 dakia alizopata kama 10 hivi kazi aliyoifanya kubwa sana.
USHINDI MWEMBAMBA NDIO BNGWA
Wengi tumezoea kuona timu ambayo inapata ushindi mwembamba ndio bingwa na Simba inafanya hivyo ushindi wake wa bao moja na kuendelea hivyo basi wengi wanaamini Simba ndio bingwa kwa matokeo haya wameona Leicester alivyochukua ubingwa msimu uliopita , lakini bado ligi ngumu yoyote kati ya Simba au Yanga anaweza kupata ubingwa haswa kwa ukubwa wa vikosi vyao.

Note: Only a member of this blog may post a comment.