Staa wa muziki wa R&B, Jason Derulo na mpenzi wake, Daphne Joy wakiwa ufukweni.
CASA ARAMARA, Mexico
ANAPIGA kote kote! Staa wa muziki wa R&B, Jason Derulo na mpenzi wake, Daphne Joy wameonyesha kuwa wanapendana sana baada ya kuonekana wakijiachia vya kutosha huko Punta Mita, Mexico, Jumanne ya wiki hii.

Jason Derulo ambaye amewahi kutoka na msanii mwenzake, Jordin Spark
aliyedumu naye kwa miaka mitatu, sasa ameangukia kwenye penzi la mrembo
Daphne Joy ambaye ni ‘ex’ wa staa wa hip hop, 50 Cent aliyezaa naye
mtoto mmoja, Sire Jackson, 3.
Staa huyo mwenye miaka 26 ambaye kwa sasa anatisha na Ngoma ya Hello
Friday na mpenzi wake huyo aliyenaye kwa miezi minne sasa walipata
nafasi ya kujiachia vilivyo kwenye Fukwe za Casa Aramara huku
wakionyesha mapenzi ya hadharani na watu kuwashangaa.
Wakiwa huko walicheza michezo mbalimbali kama kukimbizana, kumwagiana
maji, kuendesha pikipiki zinazojulikana kama ATV pamoja na mingine
mingi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.