Thursday, August 20, 2015

Anonymous

AVRIL Kurekodi Wimbo na CHRISTINA SHUSHO..Pia Afunguka Kuhusu Kuingia Kwenye Muziki wa Injili!

Muimbaji mrembo wa nchini Kenya, Avril huenda akarekodi wimbo na muimbaji wa nyimbo za injili, Christina Shusho siku za usoni.
11326145_1451883941807003_483772601_n
Hata hivyo amedai kuwa kurekodi wimbo na msanii huyo wa Tanzania hakumaanishi kuwa anaingia kwenye muziki wa injili.
Avril alikutana na Christina Shusho wiki iliyopita kwenye hafla ya Catholic University Dreamz Come True Initiative jijini Nairobi
ambapo Shusho alimuita jukwaani alipokuwa akihudumu na kumuombea pamoja na wachungaji wengine.
“That awesome moment when Christina Shusho calls you on stage and the Pastors in the house come to pray for you…too awesome ,” aliandika Avril kwenye picha aliyoweka Instagram.
Wakiwa jukwaani wawili hao walizungumza kuhusu kufanya kazi pamoja siku za usoni.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.